JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO
TAARIFA
KWA UMMA
Taarifa inatolewa kwa umma kuwa shirika la
Tanzania Sisi kwa Sisi Foundation (TSSF) lililosajiliwa chini ya sheria ya
Mashirika Yasiyo ya Kiserikali mwaka 2011 limefutiwa usajili kuanzia tarehe 04.04.2014
kutokana kukiuka masharti ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya mwaka
2002 na sheria mbalimbali za nchi. Kwa
taarifa hii, utendaji kazi wa shirika hili unasitishwa kwa mujibu wa Sheria ya
Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Namba 24, 2002 na utendaji kazi wake baada ya
taarifa hii utakuwa ni kinyume cha sheria.
IMETOLEWA
NA MSAJILI WA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI.

No comments:
Post a Comment